Stadi za Kiswahili – Mwongozo wa Mwalimu 7

KSh280.00

Stadi za Kiswahili – Mwongozo wa Mwalimu 7
Author: Mwalimu Kipande
ISBN: 978 9966 347 42 8
Kila Kitabu cha Mwalimu kinakusudia kumwelekeza mwalimu kuhusu utaratibu mwafaka wa kufuata ili aweze kufikia lengo katika kila funzo. Aidha, kinadhamiriwa kumsaidia mwalimu kuwasilisha maarifa kwa mwanafunzi kwa njia bora zaidi. Baadhi ya manufaa ya miongozo ya walimu ni pamoja na:
? Kumpangia mwalimu mada za kila muhula
? Kumbainishia mwalimu mada kuu na ndogo kama ilivyopendekezwa katika silabasi
? Kumworodheshea mwalimu malengo ya kila funzo
? Maelezo kuhusu mbinu na utaratibu wa kufundisha mada zilizomo katika Kitabu cha Mwanafunzi
? Nyenzo zihitajikazo katika kila funzo
? Maelekezo ya ziada kwa mwalimu
? Mazoezi ya ziada
? Majibu ya mazoezi yote yaliyomo katika Kitabu cha Mwanafunzi.
? Miongozo ya walimu pia ina vielelezo vya jinsi ya kupangia mafunzo ya darasa husika na pia mfano wa jinsi ya kupanga funzo.

Customer Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Stadi za Kiswahili – Mwongozo wa Mwalimu 7”

Your email address will not be published. Required fields are marked *