Dira Ya Kiswahili 8
KSh790.00
DIRA YA KISWAHILI 8 kimeandikwa kumsaidia mwanafunzi na mwalimu. Kimezingatia stadi za lugha tano: Kusikiliza na kuongea, Kusoma, Sarufi, Msamiati na Kuandika. Katika kiwango hiki, ni muhimu mwanafunzi kujenga na kukuza stadi za lugha ili kujiamini na kukomaa katika Kiswahili. Muundo wa kitabu 1. Kuna sura 15: Kila sura ina sehemu ya Kusikiliza na kuongea, Kusoma, Kuandika, Sarufi na Msamiati. 2. Baada ya kila sura kuna Kibindo cha maswali. Sehemu hii imejumlisha maswali kutoka sehemu mbalimbali na yanakuza stadi za lugha. 3. Mwisho wa kila sura kuna Zoezi la kiada. Katika sehemu hii kuna Kifungukate na Maswali mseto yanayozingatia silabasi. 4. Kuna mihula mitatu. Kila muhula una Sura tano na Jaribio la mtihani. 5. Baada ya sura kumi na tano kuna Majaribio ya mitihani kumi na mawili na Mazoezi ya nyongeza. Majaribio haya yamezingatia silabasi na muundo wa KCPE. Mazoezi ya nyongeza nayo ni ya kudadisi makali ya mwanafunzi. 6. Mwisho ni Majibu ya mazoezi na majaribio ya mitihani yote. Mwandishi wa kitabu hiki ni Wafula Wa Wafula na John Muriuki Gikunju. Wao ni mahiriri na walimu wenye tajiriba na watajika katika uwanja wa Kiswahili.
Customer Reviews
There are no reviews yet.
Be the first to review “Dira Ya Kiswahili 8”